Published - Sat, 18 May 2024

MAJADILIANO KUHUSU MAADA YA MIFANO YA MBINU SHIRIKISHI

MAJADILIANO KUHUSU MAADA YA MIFANO YA MBINU SHIRIKISHI

Pamoja na ukweli kbwamba mbinu shirikishi zinaweza kuwa chombo chenye nguvu cha kuboresha ufundishaji na ujifunzaji. Kwa maandalizi, usimamizi makini, na utofautishaji, walimu wanaweza kutumia mbinu shirikishi kuunda mazingira ya kujifunza yenye ushirikishwaji na yenye ufanisi kwa wanafunzi wote. Je ni  changamoto gani zinazoweza kutokea wakati wa kutumia mbinu shirikishi katika ufundishaji?

Created by

Math Centre

mathcentre.ac.tz adminĀ 

View profile

Comments (23)

Yohana Mapumba
Yohana Mapumba
Mbinu shirikishi ni mbinu nzuri sana katika mchakato mzima wa ufundishaji na ujifunzaji kwani huchochea sana ari ya uelewa kwa walengwa.
Thu, 13 Jun 2024
joseph mabimbi
joseph mabimbi
Mbinu shirikishi zinapotumika huwapa fursa wanafunzi kuchangia mawazo yao wakati wa majadiliano na hii hukuza ari ya kujifunza na kujiamini zaidi
Fri, 07 Jun 2024
Aloyce Charles
Aloyce Charles
Mbinu shirikishi ni zile mbinu zote zinazomfanya mkufunzi na mwanachuo kujifunza kwa ueledi wa hali ya juu na kufikia stadi muhimu zilizokusudiwa. mfano wa mbinu hizo ni:-
1. Michezo
2. Nyimbo
3. Maswali na majibu
4. Kisa mafunzo
5. Matembezi ya garali
6. Hadithi
7. Ziara na nyinginezo nyingi za kufafana na hizi.
Fri, 31 May 2024
 JOSEPHINE HIZZA
JOSEPHINE HIZZA
mbinu shirikishi ni nyenzo muhimu sana katika ujifunzaji na ufundishaji somo la hisabati,hivyo ni vyema wakufunzi tukazitumia ili na wanachuo wetu wapate uelewa na kuzitumia .
Thu, 30 May 2024
Yohana Mapumba
Yohana Mapumba
Mbinu shirikishi hutumika sana katika mchakato mzima wa ufundishaji na ujifunzaji katika somo la hisabati kwa mfano tunapotoa kazi za majadiliano, kuimba nyimba zinahusiana na hisabati n.k
Mon, 27 May 2024
STEDIUS  KAZINDUKI
STEDIUS KAZINDUKI
Mbinu hizi ni nzuri zinapotumika katika ufundishaji maandalizi mazuri ya mkufunzi yataifanya mbinu ionekane kuwa kweli ni shirikishi pia kuwepo Kwa zana Kila unapotumia mbinu ufanikisha zaidi ufundishaji shirikishi.
Mon, 27 May 2024
Adam Kaduri
Adam Kaduri
Mbinu hii ni nzuri kwa kufundishia walimu tarajali ili waweze kwenda kufundisha wanafunzi kwa kufuata taratibu na mbinu hizi zinasaidia kufanya mwanafuzi awe ndiy mtendaji wa somo kuliko mwalimu.
Mon, 27 May 2024
Adam Kaduri
Adam Kaduri
Mbinu hii ni nzuri kwa kufundishia walimu tarajali ili waweze kwenda kufundisha wanafunzi kwa kufuata taratibu na mbinu hizi zinasaidia kufanya mwanafuzi awe ndiy mtendaji wa somo kuliko mwalimu.
Mon, 27 May 2024
Adam Kilamlya
Adam Kilamlya
Mbinu shirikishi inamusaidia mwalimu tarajali kukumbuka zaidi
Mon, 27 May 2024
Alinanine Kapula
Alinanine Kapula
Mbinu shirikishi isipotumiwa vizuri unaweza kuona wachuo wenye uelewa sana wakatawala kundi, mbinu shirikishi ni zuri kuunda kundi kulingana na uwezo na genda na ili kila mmoja ashiriki uwasilishaji usichaguliwe na wanafunzi wenye unatakiwa kuchagua bila kujali na wapewe taarifa kuwa shiriki mimi ndiye nitakaye chaghua wa kuwashilisha
Sun, 26 May 2024
Yohana Mapumba
Yohana Mapumba
Mbinu shirikishi nashauri itumike zaidi katika mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji kwani wanachuo hufurahia sana somo na kuelewa zaidi.
Thu, 23 May 2024
oscar kilangi
oscar kilangi
mwezeshaji alihitaji kueleza kwa kifupi kuhusu mbinu za ufundishaji kabla mbinu shirikishi
Thu, 23 May 2024
dolia julius
dolia julius
changamoto inayojitokeza ni namna mkufunzi anavyoitumia hiyo mbinu wakati wa ufundishaji na ujifunzaji sababu akitumia vibaya hapo ndo ushirikishi unapotea mfano majadiliano kwa vikundi
Thu, 23 May 2024
Adam Chaula
Adam Chaula
Nawaza kwa sauti tu! Hivi majadiliano ya darasa nzima nayo inaweza kuwa mbinu? kama tuna mbinu ya majadiliano katika vikundi vidogo.
Thu, 23 May 2024
ARCARD MWAMLIMA
ARCARD MWAMLIMA
Endapo hawata ongozwa vizuri mfano kwa majadiliano yao katika vikundi, wanafunzi wanaweza kuanza kujadili mambo yao mengine.
lakini pia kama darasa au idadi ya wanafunzi ni kubwa katika darasa basi mwezeshaji au mwalimu anaweza kushindwa kutoa mrejesho kwa kundi mmoja mmoja na hatimaye muda kuisha
Thu, 23 May 2024
MARCO JOHN
MARCO JOHN
1. Wanafunzi kutoshiriki kikamilifu iwapo hakutakuwa na maelekezo sahihi yatakayowafanya wanafunzi washiriki mchakato wa kujifunza
2. wanafunzi wengine wanaweza kujifanya kuwa wao ni wajuaji iwapo mwalimu hatakuwa makini
Wed, 22 May 2024
ALICE P. MAKUNGANYA
ALICE P. MAKUNGANYA
Mbinu shirikishi ni muhimu sana kwa walimu tarajali na wakufunzi katika kukuza mazingira yenye ushirikiano na mafanikio darasani. Mbinu hizi huchangia kujenga uhusiano mzuri kati ya mkufunzi na walimu tarajali, kukuza ujifunzaji wa kina, na kukuza uwezo wa wanafunzi kufikiri kwa ubunifu pia kuleta ufanisi mkubwa darasani na kusaidia wanafunzi kufikia ukuaji wa kitaaluma na kibinafsi.
Wed, 22 May 2024
GAUDENCE VINCENT
GAUDENCE VINCENT
Baadhi ya walimu tarajali wanaweza kutawala majadiliano, na kuwazuia wengine kushiriki. Hii inaweza kuwa tatizo hasa kwa walimu tarajali ambao ni waoga au wenye aibu
Wed, 22 May 2024
Aloyce Charles
Aloyce Charles
Mbinu shirikishi ni changamshi katika hatua zote za ufundishaji na ujifunzaji
Wed, 22 May 2024
Yohana Mapumba
Yohana Mapumba
Mbinu shirikishi humfanya wanachuo/mkufunzi kushiriki kikamilifu katika mchakato mzima wa ufundishaji na ujifunzaji.
Wed, 22 May 2024
Elias Bosco
Elias Bosco
Mbinu shirikishi ni nzuri mnooo maana inamfanya mwanafunzi kujifunza kwa kutenda badala ya kutendewa na mwalimu
Wed, 22 May 2024
SATURININO KIGAVA
SATURININO KIGAVA
Matumizi ya mbinu shirikishi na ufanisi wa mbinu hizi hutegemea sana umahiri wa mwalimu husika katika kuzingatia hatua za kutumia mbinu husika hivyo changamoto zinazoweza kujitokeza endapo mwalimu hatafuata hatua ipasavyo ni
1.kutumia muda mwingi katika jambo dogo
2. kutoka nje ya malengo
2.
Wed, 22 May 2024
Paul Majani
Paul Majani
Mbinu shirikishi zikikosa usimamizi mzuri/matumizi sahihi wakati wa ufundishaji na ujifunzaji unaweza kusababisha kutofikiwa kwa malengo tarajiwa.
Sat, 18 May 2024
Search
Popular categories
Latest blogs