Published - Sat, 18 May 2024

MAJIDILIANO KUHUSU DHANA YA MBINU SHIRIKISHI

MAJIDILIANO KUHUSU DHANA YA MBINU SHIRIKISHI

Ni muhimu kuchagua mbinu shirikishi zinazofaa kwa umri, kiwango cha uwezo, na mitindo ya kujifunza ya wanafunzi wako. Walimu wanapaswa pia kuwa tayari kubadilika na kujaribu mbinu mpya ili kupata kinachofaa zaidi kwa wanafunzi wao. Je kwa uzoefu wako kuna umuhimu gani wa kutumia mbinu shirikishi katika ufundishaji na ujifunzaji wa somo la hisabati?

Created by

Math Centre

mathcentre.ac.tz adminĀ 

View profile

Comments (36)

JOSEPH MTONGA
JOSEPH MTONGA
Mbinu shirikishi inalenga kumfanya mwanafunzi awe mhusika wa moja kwa moja katika ujifunzaji.
Tue, 04 Jun 2024
Adam Kaduri
Adam Kaduri
Mbinu hii husaidia sana wanafunzi waweze kushirikiana kwa pamoja na kufanya darasa kuchangmka, pia humsaidia mwanafunzikujenga kumbukumbu ambayo haiwezi kufutika kichwani mwake.
Humsaidia kujiamini katika mambo mengi hivyo mbinu hii ni muhimu sana iitumika kuwa ukamilifu.
Mon, 27 May 2024
Alinanine Kapula
Alinanine Kapula
Kuna umuhimu mkubwa wa kutumia mbinu shirikishi hii ni kwasababu ukisikia ni rahisi kusaha, ukiona ni rahisi kukumbuka na ukifanya ni rahisi kuelewa hivyo mbinu shirikishi inampa nafasi ya kufanya au kutenda anachojifunza na kupata uelewa na kuongeza ubunifu
Sun, 26 May 2024
STEDIUS  KAZINDUKI
STEDIUS KAZINDUKI
Mbinu shirikishi ni muhimu katika ufundishaji Kwani uwafanya watoto kuchangamka wakati wa kujifunza. Mbinu hii ukuza vipaji mbalimbali mbalimbali vya wanafunzi. Mfano uwezo wa kujenga hoja au kujieleza,kuvumilia na kuvumiliana.
Sat, 25 May 2024
Adam Kilamlya
Adam Kilamlya
Participatory methods enhance understanding for trainee teachers and help build lasting memories, for example when they use games, songs, etc., in learning
Thu, 23 May 2024
JAMES MWANDEPU
JAMES MWANDEPU
UTANGULIZI
Matumizi ya mbinu shirikishi katika ufundishaji na ujifunzaji wa somo la hisabati ni muhimu sana kwa sababu zifuatazo;

1. Kujenga Uelewa wa Kina
Mbinu shirikishi huwapa walimu tarajali fursa ya kujadili na kushirikiana mawazo yao. Hii inasaidia kujenga uelewa wa kina wa dhana za hisabati kwa sababu wanafunzi wanashirikiana na kuelezea njia zao za kufikiria.

2. Kuongeza Ushiriki wa Wanafunzi
Mbinu hizi huchochea walimu tarajali kuwa hai na kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kujifunza. Wakati wanafunzi wanapewa nafasi ya kuchangia mawazo yao, wanakuwa na ari na motisha ya kujifunza.

3. Kukuza Ujuzi wa Kutatua Matatizo
Hisabati ni somo linalohusisha utatuzi wa matatizo. Kwa kutumia mbinu shirikishi kama vile kazi za vikundi, walimu tarajali wanajifunza jinsi ya kushirikiana na wenzao, kubadilishana mawazo, na kupata ufumbuzi wa pamoja. Hii inakuza ujuzi muhimu wa kutatua matatizo ambao ni muhimu hata nje ya darasa.

4. Kuzingatia Tofauti za Wanafunzi
Walimu tarajali wanatofautiana katika mitindo ya kujifunza, viwango vya uwezo, na uzoefu wao wa awali. Mbinu shirikishi zinatoa fursa ya kutumia njia mbalimbali za ufundishaji ambazo zinaweza kukidhi mahitaji ya wanafunzi wengi. Kwa mfano, walimu tarajali wengine wanaweza kuelewa vizuri kupitia majadiliano, wengine kupitia vitendo vya kimatumizi, na wengine kupitia uchunguzi binafsi.

5. Kuboresha Mahusiano ya Kijamii
Ufundishaji wa hisabati kwa mbinu shirikishi husaidia walimu tarajali kujenga mahusiano mazuri na wenzao. Wakati wa kushirikiana katika vikundi, wanafunzi hujifunza ujuzi wa kijamii kama vile ushirikiano, mawasiliano, na uvumilivu.

6. Kutoa Maoni ya Haraka
Katika mazingira ya mbinu shirikishi, wakufunzi wanaweza kupata maoni ya haraka juu ya uelewa wa walimu tarajali. Hii inawawezesha walimu kurekebisha mbinu zao za kufundisha kulingana na mahitaji ya walimu tarajali. Kwa mfano, kama kundi kubwa la walimu tarajali halielewi dhana fulani, Mkufunzi anaweza kurudi nyuma na kuelezea tena kwa njia tofauti.

HITIMISHO
Kwa ujumla, matumizi ya mbinu shirikishi katika ufundishaji wa hisabati siyo tu yanaboresha uelewa wa walimu tarajali, bali pia yanajenga mazingira ya kujifunza ambayo yanahamasisha ushiriki, ujuzi wa kijamii, na uwezo wa kutatua matatizo. Hii inapelekea matokeo bora ya kujifunza na maendeleo ya jumla kwa walimu tarajali
Thu, 23 May 2024
Mbinu shirikishi ni nzuri kwani inamshirikisha mwalimu na anakuwa na uelewa wa maudhui kwani yeye mwenyewe anashiriki vyema. kama nyie wawezeshaji mnavyotushirikisha tubaelewa vizuri sana,
Thu, 23 May 2024
Alinanine Kapula
Alinanine Kapula
You hear you forget, you see you remember and you do you understand. For this case interactive method is inevitable in order to make the student teacher understand
Thu, 23 May 2024
James Sospeter
James Sospeter
Mbinu shirikishi inajenga stadi za mawasiliano na ushirikiano.
Thu, 23 May 2024
Gaudis Ephraim
Gaudis Ephraim
Mbinu shirikishi hi muhimu sana Ili kufikia lengo la ufundishaji na ujifunzaji kwa wakati na kwa undani katika Somo husika.
Updated Thu, 23 May 2024
ARLON MWAKALEBELA
ARLON MWAKALEBELA
Mbinu shirikishi huongeza uelewa na urahisi katika kujifunza somo la Hisabati.
Thu, 23 May 2024
SHILINDE MALIFEDHA
SHILINDE MALIFEDHA
Mbinu shirikishi inamsaidia mwalimu tarajali kupata umahiri uliokusudiwa kwa urahisi
Thu, 23 May 2024
Alinanine Kapula
Alinanine Kapula
Mbinu shirikishi inamsaidia mwalimu tarajari kuwa n auelewa na kumbukumbu pindi anataka kuitumia
Thu, 23 May 2024
Adam Mafworo
Adam Mafworo
ushirikishwaji wa wanachuo huwa ni mkubwa katika ujifunzaji
Thu, 23 May 2024
Beno Silwani
Beno Silwani
Mbinu shirikishi hufanya mwanafunzi kuwa makini na msikivu
Thu, 23 May 2024
Baraka  Kabigi
Baraka Kabigi
kwa namna gani Mr. beno
Thu, 23 May 2024
Mbinu shirikishi ni nzuri sana kwani mwalimu tarajali anapata uelewa mzuri na anashiriki kama kitovu cha ufundishaji na ujifunzaji.
Thu, 23 May 2024
Richard Masolwa
Richard Masolwa
Mbinu shirikishi ni nzuri sana, lakini umakini katika usimamizi unahitajika.
Thu, 23 May 2024
George  Mwakisole
George Mwakisole
Mbinu shirikishi pia zinamfanya mwanafunzi awe na kumbukumbu ya kudumu
Updated Thu, 23 May 2024
dolia julius
dolia julius
Mbinu shirikishi huongeza uelewa kwa walimu tarajali na kuwajengea kumbukumbu ya kudumu mfano wanapotumia michezo katika kujifunza, nyimbo n.k
Thu, 23 May 2024
Adam Chaula
Adam Chaula
Somo zuri
Wed, 22 May 2024
Gervas Ndove
Gervas Ndove
Mbinu shirikishi huongeza Ushiriki wa walimu tarajali kama vile michezo, shughuli za kikundi na matumizi ya teknolojia huweza kuifanya hisabati iwe ya kufurahisha na kuvutia wengi kushiriki.
Wed, 22 May 2024
Yohana Mapumba
Yohana Mapumba
Kuna umuhimu mkubwa sana kujifunza mbinu shirikishi kwa sababu huwafanya wanachuo wasilale darasani wakati kipindi kinaendelea.
Wed, 22 May 2024
Yohana Mapumba
Yohana Mapumba
Ni mbinu nzuri sanaa kwani wanachuo huwa wanafurahia kipindi kwa sababu ya ushirikishwaji katika kila hatua.
Wed, 22 May 2024
Aloyce Charles
Aloyce Charles
Mbinu shirikishi inawalazi mkufunzi na wanachuo wote kwa pamoja kuwa wadadisi, wachangamfu, waona mbali katika kutatua changamoto zinazojitokeza papo kwa hapo
Wed, 22 May 2024
Elias Bosco
Elias Bosco
Ni njia nzuri mnoo katika kujifunza kwa sababu kipindi hiki ni kipindi ambacho mwanafunzi/ mwanachuo anatakiwa kuwa mtendaji mkuu bali mkufunzi anakuwa kama mwezeshaji.
Wed, 22 May 2024
Baraka  Kabigi
Baraka Kabigi
kweli kabisa Mwanachuo/mwanafunzi akiwa yeye ndeye mtendaji mkuu anakuwa na uwezo wa kukuza uwezo wake wa kufikiri na kuwa mdadisi zaidi
Thu, 23 May 2024
ZERA MSIMBE
ZERA MSIMBE
Mbinu shirikishi inamuongezea mwalimu tarajali uwezo wa kufikiri na ubunifu.
Wed, 22 May 2024
GAUDENCE VINCENT
GAUDENCE VINCENT
Mbinu Shirikishi na Uchopekaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika ufundishaji na ujifunzaji wa hisabati ni muhimu sana katika kuboresha uelewa na ufanisi wa wanafunzi. Kwa kuzingatia mbinu hizi na teknolojia inayobadilika kila wakati, ufundishaji na ujifunzaji wa hisabati unaweza kuwa wa kusisimua zaidi na wenye ufanisi zaidi kwa wanafunzi.
Wed, 22 May 2024
MASUD ALLY
MASUD ALLY
Nimependa uwasilishaji. Presenter amejitahidi kuweka maneno machache kwenye slides zake badala yake amejitahidi kudadavua dhana kwa kina. pia nimependa namna shughuli za ujifunzaji zilivyo tengenezwa.
Updated Wed, 22 May 2024
Adam Kaduri
Adam Kaduri
Picha ni nzuri sana mmejitahidi sana
Wed, 22 May 2024
MASUD ALLY
MASUD ALLY
Ndio kaka napenda kujua software inayotumika kutengeneza video hizi.
Wed, 22 May 2024
ALICE P. MAKUNGANYA
ALICE P. MAKUNGANYA
Mbinu shirikishi na uchopekaji wa TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji wa hisabati unaweza kusaidia kuchochea ujuzi wa kufikiri wa wanafunzi, kukuza ujuzi wa kiteknolojia, na kuwapa wanafunzi njia tofauti za kuelewa na kushughulikia masomo ya hisabati
Wed, 22 May 2024
SATURININO KIGAVA
SATURININO KIGAVA
Mbinu shirikishi husaidia ujifunzaji shirikishi (collaborative learning)
Wed, 22 May 2024
Baraka  Kabigi
Baraka Kabigi
Mbinu shirikishi inakuza udadisi kwa walimu tarajari pia inawafanya walimu tarajali wafikiri kwa kina kwa kuwa kila mmoja anapewa anafasi ya kuchangia mawazo yake.
Wed, 22 May 2024
MASUD ALLY
MASUD ALLY
kweli kabisa mwandamizi
Wed, 22 May 2024
MARCO JOHN
MARCO JOHN
Humwezesha mwanachuo kushiriki kikamilifu kujifunza
Huwezesha urejeshaji wa mrejesho wa pamoja
Mwanafunzi huwa na ushirikiano na wenzake, na materials pamoja na mwalimu wake
Wed, 22 May 2024
SATURININO KIGAVA
SATURININO KIGAVA
Hongera kwa uwasilishaji mzuri, nina maoni kwenye activity ya mchoro kuna mahali pameandikwa choro badala ya mchoro
Updated Wed, 22 May 2024
Andrew  Binde
Andrew Binde
Mbinu shirikishi hupunguza wanachuo wachache kupora mjadala kwa vile wote wana fursa sawa. kuchangia
Wed, 22 May 2024
Paul Majani
Paul Majani
Mbinu shirikishi ni muhimu kwani huwasaidia walimu tarajali katika ujifunzaji wao
Sat, 18 May 2024
Search
Popular categories
Latest blogs