Last updated Mon, 20-May-2024
20 Lessons
02:47:51 Hours
English
Ufundishaji na ujifunzaji unapaswa kuhusisha mbinu shirikishi ili kumwezesha mwanachuo kujenga maarifa, stadi na mwelekeo uliokusudiwa. Matumizi ya mbinu shirikishi humpa mwanachuo nafasi ya kushiriki kikamilifu katika mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji. Ni muhimu mkufunzi kuandaa mazingira bora ya ujifunzaji ili kuchochea ari ya udadisi na ubunifu wakati wa ujifunzaji. Hivyo, sehemu hii imelenga kuboresha uelewa wa mkufunzi katika kuandaa shughuli mbalimbali pamoja na mbinu shirikishi za ufundishaji na ujifunzaji wa mada za somo la Hisabati ngazi ya astashahada (mfano: jometri, aljebra, takwimu, namba kamili, sehemu, faida na hasara, seti na namba nzima).
- Kubainisha mbinu shirikishi zinazoleta ufanisi katika ufundishaji na ujifunzaji wa somo la hisabati
- Kuandaa shughuli za ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Hisabati zinazomshirikisha mwalimu tarajili katika mchakato wa ujifunzaji.
- Kutumia mbinu shirikishi katika ufundishaji na ujifunzaji wa mada chaguzi za somo la Hisabati
Write a public review